Wednesday, 7 August 2019

USIPIME UPENDO KWA

1: Kuangalia mara ngapi amekupigia simu kwa siku, kwani wapo walio pigiwa kutwa nzima, lakini bado walikuwa wakiandaliwa kihisia ili apate kile anachotaka alafu anaondoka mazima mazima.

2: kwa kuangalia vitu vya thamani unavyopewa, kwani mwingine huitazama dhiki ulio nayo na ndio uitumia kama chambo, kuwa makini katika kujieleza kwako, kwani nafsi na UTU WAKO ni vya thamani na moyo huugua sana pale unapogundua ulirubunika kwa mtu uliye jiachilia kwake na kumbe yeye alikua mpitaji.

3: kwa kudumu miaka mingi kwenye uchumba, mwingine anaitaji umsindikize katika safiri yake ili baadaye aje atulie na chaguo lake.

4: kwa majuto alio onesha ulipomsimulia historia ya maisha yako ya kale, wala usizame mazima sababu ya kuvutiwa na historia ya mtu

5: kwa kuwa tayari umempa penzi ukadhani ata data na kudumu nawe, uwenda hiyo ndio ikawa njia ya kumpa tiketi ya kuondoka.

NB: Tazama nia usitazame huruma yake tu, wakati wamuitaji akupigie ama akusaidie, au hata adumu nawe yote haya hayamfanyi MTU kudumu nawe.
Bali akiwa na KIASI kwa kila jambo, akionyesha UTU wake wa dhati bila kuongeza chumvi, akiwa na nia ya kweli huku akiithinitisha kwa matendo ya kweli na akifatisha utaratibu, hakika mtafika mahala pale Mungu anataka muwe.

"Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa kwa msaada wa kila kiungo kwa kadiri ya utendaji wa kila wa kila sehemu moja moja huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo."
(Wafilipi 4:15-16,)

Projestus.kashaija.mjuni

No comments:

Post a Comment