Sunday, 17 July 2016

SIFA MPYA YA KUJIUNGA VYUO VIKUU 2016/2017

Na,
    PROJESTUS MJUNI
-Dar es salaam
     TUME ya vyuo vikuu Tanzania TCU imetangaza upya utaratibu wakujiunga na elimu ya vyuo vikuu kwa watainia wa mwaka wa masomo 2016/2017 wanao chukuwa shahada huku wanafunzi wengi wakiwa hatarin kukosa nafasi ya masomo kutokana kukosa sifa na vigezo

             Utarstibu huo mpya umekuja ikiwa ni miezi miwili sasa tangu kutumbuliwa kwa watendaji katika tume iyo ya TCU kutokana na kudahili wanafunzi wasio na sifa na kusababisha kupewa mkopo na bodi ya wanafunzi  wa elimu ya juu HESLB

            Sifa hizo ziliwekwa mapema wiki hii katika tovuti ya TCU na kurudiwa tena.Taarifa taarifa iyo inaonesha kutolewa na kaimu mtendaji wa tume iyo eliuta mwageni
Akizungumza na mtanzania jumapili kea njia ya simu ofisa habari mwandamizi wa TCU,Edward mkaku alithibitisha taarifa ya utaratibu huo mpya

           Mkaku alisema utaratibu huo ulitolewa baadaya mwaka jana kutumika kwa mfumo wa wastani  wa GPA ambao januari mwaka huu.waziri wa elimu ,sayansi,tenchnology na mafunzo ya ufundi ,profesa joyce ndalichako  aliagiza ufutwe na kurudisha mfumo wa zamani wa division ulio kuwa unatumika siku zote

           Mfumo wa udahili ulio tumika mwaka jana  ulikuwa ni wa GPA na mwaka huu utatumika wa division  ndiyo maan utaratibu huo ukawekwa alisema mkaku

           Moja ya sifa zilizotakiwa katika udahili wa mwaka huu wa masomo 2016/2017,ni wahitimu wa kissdato cha sita waliomaliza kabla ya mwaka 2014 kuwa na ufaulu  wa D mbil,point 4.0 mchanganyuo ulionesha  kuwa point hizo zina tokana na ufaulu wa A=5 ,B= 4 C, =3 D= 2 F=1

           Taarifa hiyo inaonesha kuwa wahitimu wa kidato cha sita kwa mwaka 2014 na 2015 wawe na sifa za kudailiwa wanatakiwa wawe na sifa  wa alamaza ufaulu  wa C mbili pint 4.0 kupitia mchanyuo wa A=5 B+=4 B=3 C=2 D=1

           Pia tovuti hiyo ilionesha kuwa waitimu wanaomaliza kidato cha sita kwa mwaka huu wanahitajika  kuwa na ufaulu wa alamaD mbil 4.0 kupitia mchanganyuo wa A=5 B=4 C=3 D=2 F=1. Mbali na hzo sifa watakao dahiliwa ni wale pia watakuwa na utambulisho wa sifa za kielimu za kidato cha nne ambao ni kuanzia alama 4 za D na kupanda  juu katika mchanganuo wa alama za ufaulu wa B,ikiwa A=75-100,B+=65-74,B=50-64,C=40-49,D=35-39,F=0-38

           Sifa nyingine zinazo takiwa ni wenye cheti cha NVA daraja la tatu pamoja na ufaulu wa si chini ya alama D nne za kidato cha nne au sifa nyingine zinazo karibiana na hizo ,ikiwa ni pamoja na zinazo tambuliwa na Baraza la taifa la mitiani NECTA au mamlaka ya elimu na ufudi stand VETA

          Pia watainiwa wanatakiwakuwa na angalau  GPA ya 3.5 ya NTA stashahada NTA daraja la sita au wastani  wa B kwa cheti cha ufundi FTC katika mchanganuo wa A=5 B=4 C=3 na D=2 au wastani wa daraja la B+ kwa wenye sifa stashahada za ualimu au wastani wa daraja B+ kwa kitengo cha afya kama tabibu wa magonjwa ya binadamu na nyinginezo

          Sifa nyingine zinazo angaliwa katika udahili nipamoja na kuwa na ufaulu wa daraja la pili kwa wenye sifa za stashahada zisizo kuwa na NTA.Pamoja na hayo TCU ilisema  hakutakuwa na usajiri wa mafunzo y awali pamoja na yale ya UQF6 yaliyozuhuliwa kuanzia mwaka wa masoo wa 2016/2017.Taarifa ya tovuti iliendelea kusema kuwa maombi yote ya usajili wa wanafunzi hao wanaotaka kuchukuwa shahada yanatakiwa kupitia TCU pekee,

          Kwamba tume hiyo imeamua kuwa kuanzia mwaka 2016/2017,maombi yote ya usajili kwa makundi yote yanayoanzia  ya3.0 kwenda juu wataunganishwa naTCU pekee na walio chini ya hapo hawatahusika na tume hiyo,alisema taarifa hiyo

          Pia  TCU alisema taarifa hiyo kwa mujibu wa kipengele cha 50(i)(c)(i) cha katiba ya vyuo vikuu kifungu cha 346 cha sheria nchini.Msingi wa kubadili viwango ivyo vya kujiunga na elimu ya juu nikutoka na na kuwepo kwa maoni mbali mbali ya wadau wa elimu juu ya uwezo wa wahitimu wanaojiunga na vyuo vikuu mbalimbali ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Writer     by
                                     
                         PROJESTUS.K. MJUNI
                         P.O.BOX 100008
                         DAR ES SALAAM
                         E-MAIL;PROJESTUSMUJUNI@GMAIL.COM
                         TEL.0654639661