Elizabeth michael agosti 6,2019 afunguka kuhusu ndoa yake...
* Lulu Michael ambaye ni mwingizaji wa bongo movie ..amefunguka kuhusu ndoa yake huku akitumia mistari ya Biblia Takatifu kwa kusema kuwa ipo katika Mathayo 25:1-13.
Dar es Salaam. Mwigizaji Lulu Michael ameongea kuhusu ndoa yake huku akitumia mistari ya Biblia Takatifu na kusema kuwa ipo katika Mathayo 25:1-13.
Elizabeth ameeleza hayo jumanne Agosti 6, 2019 kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram baada ya kuulizwa swali na mchungaji Mashimo aliyetaka kujua atafunga ndoa lini.
Kiongozi huyo wa dini alitaka kujua jambo hilo akijenga hoja kuwa toka kutangazwa kwa ndoa ya mwigizaji huyo mwaka unakaribia kuisha.
Lulu alivalishwa pete ya uchumba Septemba 30, 2018 na mfanyabiashara Francis Siza maarufu Majizo ambaye ni mmiliki wa EFM redio na TVE.
Akimjibu Mchungaji Mashimo kupitia ukurasa wake huo Lulu amesema, “Kaka yangu jibu la ndoa yangu linapatikana katika kitabu cha Mathayo 25:13 na useme Ameen.”
Kwa mujibu wa andiko hilo mstari wa 13 unasema ‘Basi kesheni kwa sababu hamuijui siku wala saa.”