Na PROJESTUS MJUNI,
Serikali imetangaza orodha ya wanafunzi ambao watarejea na masomo katika chuo kikuu cha UDOM baada ya uchambuzi kumalizika na kupatikana kwa wanafunzi ambao wanasifa za kuendelea na masomo.akizungumza na waandishi wa habari waziri wa elimu sayansi nateknologia ,prof.joyce ndalichako alisema kuwa kwa kipindi chote walikuwa wakifanya uchambuzi ili kuona ni wanafunzi gani walikuwa na sifa ya kusoma kozi hiyo maalum ambayo ilianzishwa kutokana na tatizo la waalimu wa sayansi.
Alisema kuwa program hiyo ilikuwa inaitaji waalimu ambao watakwenda kufundisha shule za sekondari lakini walikuwa na wanafunzi 1,210 ambao walikuwa wanachukuwa stashahada ya ualimu wa shule za msingi ambao ni kinyume na malengo na 6,595 wakichukuwa stashahada ya kufundisha shule za sekondari
Baada ya hatua kutowaondoa wanafunzi chuoni kuchukuliwa,serikali ilifanya uchambuzi wa wanafunzi hao kwalengo la kujirithisha na sifa zao, sifa zilizo takiwa ni ufaulu wa 1 adi daraja la tatu na credit mbili au zaidi katika masomo ya sayansi na hisabati
Lakini baada ya uchambuzi kufanyika katiya wanafunzi wanao somea ualimu wa sekondari 6,595 ni wanafunzi 382 pekee ndiyo wanasifa za kuendelea na masomo yao, 134 ni mwaka wa kwanza na 248 ni mwaka pili.alisema prof.joyce ndalichako
Aidha alisema kwa wengine 4586 wa mwaka wa kwanza wa program maalum wa stashahada ya ualimu wa sekondari vigezo vya ufaulu wataamishwa katika vyuo vya ualimu vya serikali ambavyo ni MOROGORO,BUTIMBA,MPWAPWA,SONGEA NA, TUKUYU kuendelea na masomo na wanafunzi 1337 wa mwaka wa pili watahamishiwa vyuo vya korogwe na kasuru,pia alisema kuwa serikali itaendelea kuwa patia mikopo wanafunzi watakao endelea kusoma UDOM,na wata rejea chuo mwezi october mwaka huu,uku wa vyuo vya ualimu watakuwa wakilipiwa ada ya 600000 kwa mwaka ambao ni ada ya vyuo hivyo,na wataripot chuo mwazi september
Kwa upande wa wanafunzi wa kufundisha elimu ya shule ya msingi profesa ndalichako alisema wanafunzi 29 wa mwaka wa pili ambao wanacheti cha daraja A la ualimu watahamishwa chuo cha ualimu kasuru ili wamalize masomo yao ila kwa gharama zao wenyewe uku wengine 1181akiwataka waombe nafasi katika vyuo vingine katika masomo ambayo wanasifa zinazo lingana nao
writer by
PROJESTUS MUJUNI
P.O.BOX 100008
DAR ES SALAAM
E-MAIL;PROJESTUSMUJUNI@GMAIL.COM
TEL,0654639661