Friday, 22 July 2016

BREAKING NEWS;USIKU WA KUAMKIA LEO TAREHE 22JULY2016 MWIGIZAJI WA VICHEKESHO ISMAIL ISSA MAKOMBE A.K.A BABA KUNDABADA AFARIKI DUNIA


Na,
  PROJESTUS MJUNI

Msanii wa vichekesho (komedi ) maarufu  kwa jina la ismail issa makombe A.K.A ,KUNDAMBANDA ,amefariki dunia usiku wa kuamkia leo

Kundambada alikuwa mgombea ubunge wa CUF na ukawa kwenye jimbo la masasi mkoani mtwara katika uchaguzi ulio fanyika  mwezi desembe 2015 baada ya ule wa oktoba kutofanyika na kifo cha aliye kuwa mgombea wa awali wa ukawa .Mhe.Emanuel Makaidi (NLD).wakati wa uchaguzi huo wa Desemba 2015.kundambanda alipata kura 14,069 dhidi ya kura16597 za (mshindi) Rashidi chua chua kutoka ccm.Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwao masasi.inna lillah wainailayna.raijun. R.I.P Kundambanda

writer by

             PROJESTUS MJUNI
             E-MAIL,projestusmujuni@gmail.com

Thursday, 21 July 2016

ELIZABETH MICHAEL (LULU) AZUNGUMZIA PICHA ALIYO POST INSTAGRAM AKIWA AMEVAA PETE YA UCHUMBA



Na,
     PROJESTUS MJUNI
     Dar es salaam

Mwigizaji wa bongo movie Elizabeth lulu alichukuwa headlines baada ya kupost picha katika ukurasa wake wa instagram picha iyo ikionesha akiwa amevaa pete ya uchumba,ikiwa imeandikwa hivi,Asante mungu kwa neema zako ambazo hazijawai kuniacha,maana hiki kitendo cha kishujaa kujinunulia pete nzuri kama hii kwa neema tu.hayo ndiyo maneno aliyo andika lulu katika page yake ya instagram

Niswali kwa wanaofatilia maisha ya mwagizaji huyu elezabeth michael wamekuwa wakijiuliza mpaka leo akijiuliza nikweli lulu alivalishwa ya uchumba lakin akaamua kuileta kwa maana nyingine ambapo hata hivyo aliifuta post hiyo muda mfupi baada ya kuipost katka page yake ya instagram ,,Huku akinena ya kuwa akuwa na sababu maalum ya kupost na kuifuta ,nilikuwa nacheza na tu na nimekuja kugundua watanzania wanapenda sana drama,nilivyo ona comments ndio nikajua ni watu wa namna gani wananifatilia,ni pete ambayo niliamua kuinunua na kuivaa

writer by
PROJESTUS MJUNI
E-MAIL,PROJESTUSMUJUNI@GMAIL.COM
TEL.0654639661










Wednesday, 20 July 2016

WANAFUNZI 382 KURUDI UDOM KATI YA YA 7,805 WARIO RUDISHA NYUMBANI,WINGI WAO WATAJWA KUCHANGIA MGOMO WA WALIMU

Na PROJESTUS MJUNI,

                        Serikali imetangaza orodha ya wanafunzi ambao watarejea na masomo katika chuo kikuu cha UDOM baada ya uchambuzi kumalizika na kupatikana kwa wanafunzi ambao wanasifa za kuendelea na masomo.akizungumza na waandishi wa habari waziri wa elimu sayansi nateknologia ,prof.joyce ndalichako alisema kuwa kwa kipindi chote walikuwa wakifanya uchambuzi ili kuona ni wanafunzi gani walikuwa na sifa ya kusoma kozi hiyo maalum ambayo ilianzishwa kutokana na tatizo la waalimu wa sayansi.

                          Alisema kuwa program hiyo ilikuwa inaitaji waalimu ambao watakwenda kufundisha shule za sekondari lakini walikuwa na wanafunzi  1,210 ambao walikuwa wanachukuwa stashahada ya ualimu wa shule za msingi ambao ni kinyume na malengo na 6,595 wakichukuwa stashahada ya kufundisha shule za sekondari

                            Baada ya hatua kutowaondoa wanafunzi chuoni kuchukuliwa,serikali ilifanya uchambuzi wa wanafunzi hao kwalengo la kujirithisha na sifa zao, sifa zilizo takiwa ni ufaulu wa 1 adi daraja la tatu na credit mbili au zaidi katika masomo ya sayansi na hisabati

                           Lakini baada ya uchambuzi kufanyika katiya wanafunzi wanao somea ualimu wa sekondari 6,595 ni wanafunzi 382 pekee ndiyo wanasifa za kuendelea na masomo yao, 134 ni mwaka wa kwanza na 248 ni mwaka pili.alisema prof.joyce ndalichako

                                   Aidha alisema kwa wengine 4586 wa mwaka wa kwanza wa program maalum wa stashahada ya ualimu wa sekondari vigezo vya ufaulu wataamishwa katika vyuo vya ualimu vya serikali ambavyo ni MOROGORO,BUTIMBA,MPWAPWA,SONGEA NA, TUKUYU kuendelea na masomo na wanafunzi 1337 wa mwaka wa pili watahamishiwa vyuo vya korogwe na kasuru,pia  alisema kuwa serikali itaendelea kuwa patia mikopo wanafunzi watakao endelea kusoma UDOM,na wata rejea chuo mwezi october mwaka huu,uku wa vyuo vya ualimu watakuwa wakilipiwa ada ya 600000 kwa mwaka ambao ni ada ya vyuo hivyo,na wataripot chuo mwazi september

                     Kwa upande wa wanafunzi wa kufundisha elimu ya shule ya msingi profesa ndalichako alisema wanafunzi 29 wa mwaka wa pili ambao wanacheti cha daraja A la ualimu watahamishwa chuo cha ualimu kasuru ili wamalize masomo yao ila kwa gharama zao wenyewe uku wengine 1181akiwataka waombe nafasi katika vyuo vingine katika masomo ambayo wanasifa zinazo lingana nao
  



writer by 
PROJESTUS MUJUNI
P.O.BOX 100008
DAR ES SALAAM
E-MAIL;PROJESTUSMUJUNI@GMAIL.COM
TEL,0654639661

Sunday, 17 July 2016

SIFA MPYA YA KUJIUNGA VYUO VIKUU 2016/2017

Na,
    PROJESTUS MJUNI
-Dar es salaam
     TUME ya vyuo vikuu Tanzania TCU imetangaza upya utaratibu wakujiunga na elimu ya vyuo vikuu kwa watainia wa mwaka wa masomo 2016/2017 wanao chukuwa shahada huku wanafunzi wengi wakiwa hatarin kukosa nafasi ya masomo kutokana kukosa sifa na vigezo

             Utarstibu huo mpya umekuja ikiwa ni miezi miwili sasa tangu kutumbuliwa kwa watendaji katika tume iyo ya TCU kutokana na kudahili wanafunzi wasio na sifa na kusababisha kupewa mkopo na bodi ya wanafunzi  wa elimu ya juu HESLB

            Sifa hizo ziliwekwa mapema wiki hii katika tovuti ya TCU na kurudiwa tena.Taarifa taarifa iyo inaonesha kutolewa na kaimu mtendaji wa tume iyo eliuta mwageni
Akizungumza na mtanzania jumapili kea njia ya simu ofisa habari mwandamizi wa TCU,Edward mkaku alithibitisha taarifa ya utaratibu huo mpya

           Mkaku alisema utaratibu huo ulitolewa baadaya mwaka jana kutumika kwa mfumo wa wastani  wa GPA ambao januari mwaka huu.waziri wa elimu ,sayansi,tenchnology na mafunzo ya ufundi ,profesa joyce ndalichako  aliagiza ufutwe na kurudisha mfumo wa zamani wa division ulio kuwa unatumika siku zote

           Mfumo wa udahili ulio tumika mwaka jana  ulikuwa ni wa GPA na mwaka huu utatumika wa division  ndiyo maan utaratibu huo ukawekwa alisema mkaku

           Moja ya sifa zilizotakiwa katika udahili wa mwaka huu wa masomo 2016/2017,ni wahitimu wa kissdato cha sita waliomaliza kabla ya mwaka 2014 kuwa na ufaulu  wa D mbil,point 4.0 mchanganyuo ulionesha  kuwa point hizo zina tokana na ufaulu wa A=5 ,B= 4 C, =3 D= 2 F=1

           Taarifa hiyo inaonesha kuwa wahitimu wa kidato cha sita kwa mwaka 2014 na 2015 wawe na sifa za kudailiwa wanatakiwa wawe na sifa  wa alamaza ufaulu  wa C mbili pint 4.0 kupitia mchanyuo wa A=5 B+=4 B=3 C=2 D=1

           Pia tovuti hiyo ilionesha kuwa waitimu wanaomaliza kidato cha sita kwa mwaka huu wanahitajika  kuwa na ufaulu wa alamaD mbil 4.0 kupitia mchanganyuo wa A=5 B=4 C=3 D=2 F=1. Mbali na hzo sifa watakao dahiliwa ni wale pia watakuwa na utambulisho wa sifa za kielimu za kidato cha nne ambao ni kuanzia alama 4 za D na kupanda  juu katika mchanganuo wa alama za ufaulu wa B,ikiwa A=75-100,B+=65-74,B=50-64,C=40-49,D=35-39,F=0-38

           Sifa nyingine zinazo takiwa ni wenye cheti cha NVA daraja la tatu pamoja na ufaulu wa si chini ya alama D nne za kidato cha nne au sifa nyingine zinazo karibiana na hizo ,ikiwa ni pamoja na zinazo tambuliwa na Baraza la taifa la mitiani NECTA au mamlaka ya elimu na ufudi stand VETA

          Pia watainiwa wanatakiwakuwa na angalau  GPA ya 3.5 ya NTA stashahada NTA daraja la sita au wastani  wa B kwa cheti cha ufundi FTC katika mchanganuo wa A=5 B=4 C=3 na D=2 au wastani wa daraja la B+ kwa wenye sifa stashahada za ualimu au wastani wa daraja B+ kwa kitengo cha afya kama tabibu wa magonjwa ya binadamu na nyinginezo

          Sifa nyingine zinazo angaliwa katika udahili nipamoja na kuwa na ufaulu wa daraja la pili kwa wenye sifa za stashahada zisizo kuwa na NTA.Pamoja na hayo TCU ilisema  hakutakuwa na usajiri wa mafunzo y awali pamoja na yale ya UQF6 yaliyozuhuliwa kuanzia mwaka wa masoo wa 2016/2017.Taarifa ya tovuti iliendelea kusema kuwa maombi yote ya usajili wa wanafunzi hao wanaotaka kuchukuwa shahada yanatakiwa kupitia TCU pekee,

          Kwamba tume hiyo imeamua kuwa kuanzia mwaka 2016/2017,maombi yote ya usajili kwa makundi yote yanayoanzia  ya3.0 kwenda juu wataunganishwa naTCU pekee na walio chini ya hapo hawatahusika na tume hiyo,alisema taarifa hiyo

          Pia  TCU alisema taarifa hiyo kwa mujibu wa kipengele cha 50(i)(c)(i) cha katiba ya vyuo vikuu kifungu cha 346 cha sheria nchini.Msingi wa kubadili viwango ivyo vya kujiunga na elimu ya juu nikutoka na na kuwepo kwa maoni mbali mbali ya wadau wa elimu juu ya uwezo wa wahitimu wanaojiunga na vyuo vikuu mbalimbali ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Writer     by
                                     
                         PROJESTUS.K. MJUNI
                         P.O.BOX 100008
                         DAR ES SALAAM
                         E-MAIL;PROJESTUSMUJUNI@GMAIL.COM
                         TEL.0654639661